Timu ya soka ya Simba sc leo hii imeanza vyema Ligi kuu ya vodacom baada ya kuifunga timu ya Ndanda fc magoli 3-1 katika uwanja wa Taifa.
Goli la kwanza la Simba sc lilifungwa na Laudit Mavugo katika dakika ya 19 lakini timu ya Ndanda fc ilichomoa katika dakika ya 36 kupitia mshambuliaji wake Omary Mponda.
Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa sare 1-1.
Katika kipindi cha pili kocha mkuu wa Simba Joseph Omog alifanya mabadiliko kwa kumtoa Ibrahim Hajib na akaingia Fredrick Blagnon. Mabadiliko hayo yalileta faida kwani Fredrick Blagnon aliweza kuifungia timu ya Simba goli la pili katika dakika ya 74 na goli la tatu la Simba sc lilifungwa na Shizya Kichuya kwa shuti kali sana liliomshinda goli kipa wa Ndanda fc Jackson Chove.
Post a Comment