SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: HAKUNA KAMA SIMBA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
KIKOSI CHA VIONGOZI WA SIMBA SIKU YA SIMBA DAY 2015 Simba hatetereki, Simba hutamba hata Jangwani achilia mbali milimani na kwenye nyika...
KIKOSI CHA VIONGOZI WA SIMBA SIKU YA SIMBA DAY 2015
Simba hatetereki, Simba hutamba hata Jangwani achilia mbali milimani na kwenye nyika ambako yeye ni mfalme. Simba hupambana, Simba huwinda bila kukata tamaa hata anapokua mgonjwa. Wajuzi husema hata akonde vipi, Simba hafanani na mbwa.

Ndugu wanasimba, hilo linadhihirishwa na sapoti ya hali ya juu ambayo tumekua tukiitoa kwa timu yetu kwenye kila aina ya nyakati. Tumekua wamoja pamoja na changamoto za hapa na pale, tukipasua milima na mabonde na hatimaye nuru imeanza kuonekana.

Tupo katika hatua nzuri ya maendeleo ya kweli. Hatua ya mabadiliko ya mfumo wa klabu yetu ambao nia na madhumuni ni kuifanya iweze kujitegemea kiuchumi. Tena uchumi ulio thabiti na imara katika dunia ya sasa.

Pamoja na ukweli kwamba kwa miaka ya hivi karibuni tumeikosa ile Simba tunayoijua, lakini walau uwanja wetu wenyewe upo katika hatua nzuri tu na ninaweza kukuhakikishia kwamba utakamilika muda si mrefu. Tuwe na uwanja wa mazoezi wa kwetu wenyewe, ni kitu ambacho kilishindikana kwa kipindi kirefu na ni kitu ambacho hata wenzetu wengi wameshindwa kufanya.

Si nia yangu kueleza hayo leo, nia yangu ni kuwakumbusha jambo hili ambalo pia limekua likidhihirisha kwamba Simba ni klabu ya watu makini. SIMBA DAY ni sikukuu yetu Wanasimba ambayo naweza kusema ni tamasha kubwa la klabu katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki.

Hakuna timu yoyote ambayo imeweza kuwa na utaratibu kama huu, na hiki ni kitu ambacho wanasimba tunapaswa kujivunia. Ni kitu kinachotuunganisha sisi, viongozi wetu na wachezaji wetu.

Hii ni Simba Week, ambapo shughuli nyingi za kuelekea kwenye kilele cha siku yetu zinafanyika. Tunafanya usafi, tunatembelea wagonjwa, tunatoa misaada na mambo mengine mengi kwa jamii yetu. Lakini kilele cha yote haya ni Agosti 8 pale uwanja wa taifa

Kilele cha siku hii ni mechi kati ya Simba na FC Leopards kutoka Kenya lakini itatanguliwa na mambo mengi kama utambulisho wa jezi zetu mpya ambazo pia zitakua zikiuzwa pale uwanjani.

Tutazitambua namba za wachezaji wetu watazozitumia kwenye msimu mpya,
Lakini pia tutakiona kikosi chetu chote siku hiyo. Wachezaji wapya wakiwemo wale wa kimataifa pamoja na wazamani ambao kwa pamoja wataunda kikosi kipya cha Simba chenye kila aina ya matumaini, watatambulishwa mbele ya Wanasimba.

Hii ni fursa ya pekee ambayo inapatikana mara moja tu kwa mwaka. Fursa ya kuwaona wachezaji wote wakitambulishwa na kisha kuwaona uwanjani wakimenyana na AFC Leopards.

Kama wewe ni mwanasimba, njoo uwanja wa taifa Agosti 8 ili uwe sehemu ya Simba itakayoandika historia mpya.
Njoo uwe sehemu ya vuguvugu la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vilabu, mfumo ambao ni sisi tunaokwenda kuuanzisha hapa nchini. Tayari wapinzani wanaweweseka na wanatamani kuiga kwa sababu wanajua Simba akiwa imara anatisha kiasi gani.

Njoo tuongee ya kwetu, tuburudike kwa pamoja kama familia kwa sababu kutakua na burudani nyingi na show zilizoandaliwa na uongozi kwa ajili yetu.
Njoo tujivunie kua Simba,

Simba Nguvu Moja


Imeandikwa na Ally shatry (Bab chicharito)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top