Kocha
Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles
Boniface Mkwasa ametangaza kikosi
kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza
na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Taifa
Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine
katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada
ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili; Taifa Stars ina pointi
moja wakati Chad ilijitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za
Tanzania kucheza fainali hizo.
Kikosi hiko kitaingia kambini kuanzia Agosti 1-5
Kikosi Kamili cha Taifa Stars:
Walinda Milango:
Deogratius Munishi, Aishi Manula, Benno Kakolanya.
Walinzi:
Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Mohamed Hussein, Juma Abdul, Erasto Nyoni.
Viungo:
Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude,
Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Hassan Kabunda, Simon Msuva.
Washambuliaji:
Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Hajib, John Bocco, na Jeremiah Juma.
MKWASA ATAJA 24 KUWAVAA NIGERIA SEPTEMBER
Title: MKWASA ATAJA 24 KUWAVAA NIGERIA SEPTEMBER
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali y...
Post a Comment