Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lingependa kutoa ufafanuzi kuwa
iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16
inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho
maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha
nchi katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.
Kwa msingi huo, timu ambayo itafungwa katika fainali hizo za Kombe la
Shirikisho –ASFC linalodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam,
ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho
Barani Afrika katika msimu wa 2016/17
Fainali za Kombe la Shirikisho zinatarajiwa kufanyika baadaye mwezi
ujao, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mchuano
uliohusisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la
Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment