Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha
Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa
12.00 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika
mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016
katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.
Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo leo Mei
18, 2016 mbele ya waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala
jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo unadumisha uhusiano na upendo wa enzi wa nchi za Kenya na
Tanzania na umeingizwa kwenye orodha ya viwango vya Shirikisho la Soka
la Kimataifa (FIFA).
Kikosi cha Stars kina makipa, Deogratius Munishi (Young Africans),
Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati
mabeki ni Mwinyi Haji na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris,
David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na
Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi
Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar),
Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda
(Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe),
Mbwana Samatta (KDC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib
(Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah
Juma (Tanzania Prisons).
TAIFA STARS KULEKEA NAIROBI KESHO
Title: TAIFA STARS KULEKEA NAIROBI KESHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho ...
Post a Comment