Beki wa kulia wa timu ya soka ya Young African ya Dar es Salaam, Juma
Abdul ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili, 2016 baada ya kura
zake kuwashinda Donald Ngoma ambaye pia anakipiga Young Africans na
Hassan Dilunga wa JKT Ruvu ya Pwani.
Katika rekodi za Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) iliyoketi Jumamosi
Iliyopita, imeonesha kwamba Abdul alicheza mechi zote tano za Ligi Kuu
kwa mwezi Aprili ambapo pia aliifungia timu yake bao katika harakati za
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/16.
Rekodi hizo pia zinaonyesha kwamba beki huyo hakuonyeshwa kadi hata
moja katika michezo hiyo mitano sambamba na kutoa mchango mkubwa katika
michezo aliyoshiriki kwa mwezi Aprili, 2016. Abdul atazawadiwa fedha Sh.
1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya mahiri
ya simu za mkononi ya Vodacom.
Uwezo aliouonyesha Abdul ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles
Boniface Mkwasa ‘Master’ kumjumuisha katika kikosi chake kwa ajili ya
mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya
kadhalika Mapharao wa Misri katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Juni 4, mwaka huu.
Wachezaji bora wa miezi minne iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa
Young Africans (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari
2016), Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016) na
Shiza Ramadhani Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi 2016).
JUMA ABDUL NDIE MCHEZAJI BORA MWEZI APRIL
Title: JUMA ABDUL NDIE MCHEZAJI BORA MWEZI APRIL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Beki wa kulia wa timu ya soka ya Young African ya Dar es Salaam, Juma Abdul ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili, 2016 baada ya ...
Post a Comment