Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki
michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza
kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.
Mashindano ya vilabu Kombe la Nile Basin huandailiwa na CECAFA kwa
kushirikisha vilabu vilivyoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi
kwa nchi wanachama wa CECAFA.
Bingwa michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi ya dola za
kimarekani U$30,000, mshindi wa pili dola U$20,000, huku mshindi wa tatu
akipata kitita cha dola za kimarekani U$10,000.
Nile Basin inashirikisha vilabu kutoka katika nchi wanachama wa
CECAFA ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan
Kusini, Tanzania na Zanzibar.
Vitoria University kutoka Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo
baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa
fainali uliofanyika mwaka 2014.
SIMBA YATHIBITISHA KUSHIRIKI KOMBE LA NILE BASIN
Title: SIMBA YATHIBITISHA KUSHIRIKI KOMBE LA NILE BASIN
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Bara...
Post a Comment