SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KAMATI YA NDIHAMU TFF YAZISHUSHA TEAM ZOTE NNE ZA KUNDI C
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimetoa  maamuzi yake leo asubuhi katika ofisi za (TFF) bila kuf...
Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimetoa  maamuzi yake leo asubuhi katika ofisi za (TFF) bila kufungamana na upande wowote

Kamati ilikutana kwa ajili ya kumalizia shauri la upangaji wa matokeo Ligi Daraja la Kwanza na kutoa hukumu ya kundi C inayozihusisha timu za Geita Gold, JKT Kanembwa, JKT Oljoro na Polisi Tabora.

 Polisi Tabora ilicheza na JKT Oljoro, Geita Gold Sports yenyewe ilicheza na JKT Kanembwa ambapo Geita ilishinda bao 8-0 wakati Polisi yenyewe iliibuka na bao 7-0. Kesi hiyo imefanyika mara tatu kwa kuwahoji viongozi wa timu, wachezaji, makocha pamoja na waamuzi na makamisaa wa mechi hizo.

Polisi Tabora na JKT Oljoro zenyewe zimeshushwa mpaka Ligi Daraja la Pili (SDL) wakati Geita nayo imeshusha hadi daraja la pili na JKT Kanembwa imeshushwa hadi ligi ya mkoa.

Waliofungiwa kuhusika na masuala ya soka maisha yao yote ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Mwenyekiti wa JKT Oljoro Amos Mwita, Kocha Msaidizi wa Tabora, Katibu wa Chama cha soka Tabora Fateh Remtullah, kocha msaidizi wa Geita, Choki Abeid na Katibu wa Polisi Tabora, Alex Kataya, mwamuzi na kamisaa wa mchezo wa JKT Kanembwa na Geita Gold Sport. 


Waliofungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 10 na faini ya Sh 10 milioni ni kpa wa Geita Denis Richard aliyewahi kuidakia timu ya vijana ya Simba na mwamuzi Hamis Mchunde, refa Masoud Mkelemi, kipa wa JKT Kanembwa, Mohamed Mohamed aliyekiri kupokea Sh 300,000.

Hukumu hiyo imesomwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Jerome Msemwa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top