Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation
Cup), inatarajiwa kufanyika kesho Jumanne saa 3 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.
Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itafanyika live
katika kituo cha AzamTwo, ambao kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu
wa michuano hiyo iliyoibua msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha
timu nyingi zaidi nchini.
Baada ya timu za Azam FC, Mwadui FC, na Yanga SC kukata tiketi ya
kucheza Nusu Fainali, mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya
Coastal Union utakaochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam atungana na timu hizo tatu kwenye droo ya kesho.
Michuano ya Kombe la Shirikisho iliyoanza kwa kushirikisha timu 64
mwishoni mwa mwaka jana, imefikia hatua hatua ya nusu fainali, baada ya
Azam FC kuindoa Prisons (3-1), Mwadui FC kuiondosha Geita Gold (3-0) na
Yanga SC kuwaondoa Ndanda FC kwa mabao (2-1).
Mshindi wa Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu huu, ataiwakilisha
Tanzania mwaka 2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
(CAF CC).
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment