SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NJOMBE: WACHEZAJI WANA MZUKA NA MECHI YA LEO YA SIMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Njombe Mji imesema wachezaji wake wapo kwenye morali ya hali ya juu kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba utakaofanyika kwenye uw...
Timu ya Njombe Mji imesema wachezaji wake wapo kwenye morali ya hali ya juu kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba utakaofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Mchezo huo ni wakiporo kufuatia Simba kupewa nafasi ya kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry wiki mbili zilizopita.

Msemaji wa klabu hiyo, Hassan Macho amesema kocha wao Ally Bushiri 'Benitez' amewaambia nyota wote wapo kwenye hali nzuri wakiahidi ushindi mbele ya Simba jioni ya leo.

Macho amesema wanaiheshimu Simba kutoka na kikosi chao na historia walionayo katika soka la nchi hii lakini leo wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kujitoa kwenye eneo la kushuka daraja.

"Tunafahamu mechi itakuwa ngumu, Simba ni timu nzuri ina wachezaji bora kwa sasa lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunabaki na pointi zote tatu nyumbani," alisema Macho.

Mchezo wa leo ni muhimu kwa timu zote kwani Simba inahitaji kushinda ili kujiwekea mazingira ya kutwaa taji msimu huu wakati Njombe wakitaka kujinasua na janga la kushuka daraja.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top