SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: BEKI WA AZAM KWENDA BONDENI JUMATATU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mlinzi wa pembeni wa Azam FC, Daniel Amoah ataenda nchini Afrika Kusini Jumatatu kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya goti. Amoah raia ...
Mlinzi wa pembeni wa Azam FC, Daniel Amoah ataenda nchini Afrika Kusini Jumatatu kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya goti.

Amoah raia wa Ghana amekuwa mhimili mkubwa upande wa kulia hasa baada ya kuondoka kwa Shomari Kapombe ambaye alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu.

Beki huyo ataongozana na Daktari wa timu Mwanandi Mwankemwa nchini humo kwa ajili ya uangalizi kwa muda wote atakapokuwa kule.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd ameiambia SDF Sports kuwa visa ya mchezaji itatoka kesho Ijumaa na safari yenyewe itakuwa Jumatatu.

"Mlinzi wetu Daniel Amoah ataenda Afrika Kusini, Jumatatu kwa ajili ya uchunguzi wa goti pamoja na matibabu akiambatana na Daktari wa timu," alisema Jaffer.

Mwezi uliopita nahodha wa timu hiyo Himid Mao nae alienda Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top