Mabingwa wa ligi kuu nchini Hispania Real Madrid imekubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Barcelona mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Madrid ipo nyuma kwa pointi 14 dhidi ya Barca hali ambayo inaonyesha wana kazi kubwa ya kufanya ili kutetea ubingwa wake.
Mshambuliaji Luis Suarez aliifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 54 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Sergio Roberto.
Lionel Messi alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 64 baada ya mlinzi Dani Carvajal kuudaka mpira uliokuwa unaelekea wavuni na kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Alex Vidal alikamilisha karamu ya mabao baada ya kupigilia msumari wa mwisho katika muda wa nyongeza kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Messi.
Barcelona wameendelea kubaki kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi 45 wakati Real wakiwa wa nne na alama zao 31.
MADRID YAZIDI KUUWEKA UBINGWA REHANI YAPIGWA NA BARCA
Title: MADRID YAZIDI KUUWEKA UBINGWA REHANI YAPIGWA NA BARCA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa wa ligi kuu nchini Hispania Real Madrid imekubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Barcelona mchezo uliofanyika kwenye ...
Post a Comment