SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: GUARDIOLA: VITA YA BINGWA EPL BADO HAIJAISHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja Pep Guardiola wa Manchester City amesema anawaonea huruma wapinzani wake lakini amesisita vita ya ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza ...
Meneja Pep Guardiola wa Manchester City amesema anawaonea huruma wapinzani wake lakini amesisita vita ya ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza bado haikwisha.

City wako kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi 13 baada ya ushindi jana wa mabao 4-0 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye uwanja wa Etihad ambapo wameshinda mechi 18 ya ligi mpaka sasa.

Manchester United ambao wanashika nafasi ya pili jana walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Leicester City nakuzidi kumsafishia njia Guardiola ya kutwaa ubingwa msimu huu.

"Kama ulinisikiliza kwa miezi 18 niliokuwepo hapa sijawahi kusema neno baya kwa wapinzani wangu. United na Chelsea wana pointi nyingi ambazo huwezi kuwatoa kwenye mbio za ubingwa.

"Ndio maana nasema bado vita ya ubingwa haijaisha sababu ukitoka sare mchezo mmoja au kupoteza mambo yanabadilika. Nawaheshimu wapinzani wangu," alisema Guardiola.

Tofauti ya pointi 13 kabla ya sikukuu ya Krismas ni historia mpya ambayo imewekwa na City tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top