SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA WAIPIGISHA DEBE STAND NA KUKAA KILELENI VPL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Napiga debe wa Stand United jioni ya leo katika uwanja wa Kambarage Mjini Sh...
Timu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Napiga debe wa Stand United jioni ya leo katika uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga

Shiza Kichuya alikuwa wa kwanza kuiandikia goli Simba Katika dakika ya 18 baada ya kuunganisha vyema pasi ya John Bocco

Mpaka mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi na Simba walimtoa Emmanuel Okwi na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavuho , Simba waliandika bao la Pili kupitia kwa Laudit Mavugo katika dakika ya 46 baada ya kuunganisha vizuri pasi ya Mzamir Yassin

Dakika ya 52 Mtasa Munashe aliipatia Stand United goli moja baada ya mwamuzi kuwapa Stand Penati Mpaka dakika 90 Stand 1-2 Simba

Ligi kuu Vodacom itasimama mpaka tarehe 14 oktoba kupisha kalenda ya fIfa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top