Pamoja na kuwa safu yao ya ushambuliaji haijafunga mabao mengi msimu huu timu ya Azam FC imepanga kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya Mbeya City kesho kwenye uwanja wao wa Azam Complex.
Azam ambayo imerejea jijini Dar es Salaam ikitokea kanda ya ziwa ilipocheza mechi mbili dhidi ya Mwadui na Mbao nakuambilia pointi mbili baada ya kuambulia sare mbili.
Ofisa habari wa klabu hiyo Jeffer Idd amesema wanaiheshimu sana Mbeya City kutokana na mabadiliko waliyofanya katika benchi la ufundi lakini wamejipanga kushinda kwa idadi nzuri ya mabao kutokana na maandalizi waliyofanya.
"Ni wazi safu yetu ya ushambuliaji haijafunga mabao mengi mpaka sasa, na hii inatokana na wachezaji wetu kuwa bado hawajazoena vizuri na mwalimu analifanyia kazi," alisema Jaffer.
Jeffer amesema timu nyingi zinazoshiriki ligi zimekuwa zikiwakamia sana kitu kinacho ambacho kinawapa wakati mgumu wachezaji wao.
Wakati huo huo Jeffer amewataka waamuzi wachezeshe kwa kufuata sheria 17 za soka ili kupunguza malalamiko ambapo kwa sasa wanajitahidi kufanya vizuri.
AZAM: TUTAWAPIGA MBEYA CITY KESHO
Title: AZAM: TUTAWAPIGA MBEYA CITY KESHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Pamoja na kuwa safu yao ya ushambuliaji haijafunga mabao mengi msimu huu timu ya Azam FC imepanga kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya Mbeya...
Itakuwa mechi nzuri sana kutizama
ReplyDelete