Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara yanga leo wameendelea na mwanzo usio wa kuridhisha sana wa msimu wa mwaka 2017/18 baada ya kulazimisha suluhu tasa mbele ya wakata miwa wa sukari mtibwa sugar.
Mechi hiyo ilokuwa ya kiushindani ilishuhudia timu zote zikishambuliana mara kwa mara lakini sifa za pekee zimwendee golikipa wa mtibwa benedict tinoco ambae alifanya kazi ha ziada kuokoa michomo ya washambuliaji wa yanga.
Pamoja na mabadiliko kadhaa ya wachezaji kwa timu zote lakini si Geodge lwandamina kocha wa yanga wala zuberi katwila kocha wa mtibwa aliyetoka na furaha.
matokeo hayo yanaiacha mtibwa kukaa kileleni kwa alama zao 11.
Matokeo mengine ya ligi hiyo leo ni kama ifuatavyo.
Ndanda 2-1 Lipuli
Mwadui 2-2 Mbeya City
Mbao 1-1 Tz Prison
Maji maji 0-0 kagera
Ruvushooting 1-1 Njombe
Singida 1-1 Azam
YANGA NA AZAM NGOMA ZACHACHA
Title: YANGA NA AZAM NGOMA ZACHACHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara yanga leo wameendelea na mwanzo usio wa kuridhisha sana wa msimu wa mwaka 2017/18 baad...


Post a Comment