SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA YAPELEKA KILIO JANGWANI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Simba wametwaa ngao ya hisani baada ya kuifunga timu ya Yanga 5-4 katika matuta, kufuatia sare ya 0-0 katika dakika tisini...
Timu ya soka ya Simba wametwaa ngao ya hisani baada ya kuifunga timu ya Yanga 5-4 katika matuta, kufuatia sare ya 0-0 katika dakika tisini.

Dakika 90 za kawaida za mchezo huo zilikamilika bila timu yoyote kupata goli, hivyo mwamuzi Elly Sassii kutoka Arusha akaamuru zipigwe penati ili kupata mshindi. 

Penati za Simba zilifungwa  na Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, Method Mwanjale, Emmanuel Okwi na Mohamed Ibrahim aliyekwamisha wavuni penati ya ushindi na penati ya Mohamed Hussein ikaishia mikononi mwa golikipa wa Yanga Rostand Youthi. 

Penati za Yanga zilifungwa  na Thabaan Kamusoko, Tshishimbi, Donald Ngoma na Ibrahim Hajib na waliokosa ni Juma Mahadhi na Kelvin Yondan.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top