Mwanamuziki
nguli wa muziki dansi nchini,Hussein juzi alijikuta akimwaga
machozi
ya furaha wakati wa mazoezi ya pamoja na mastaa wenzake wanaounda
kikosi cha timu ya Taifa dansi yaliyofanyika
katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma
Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea mara baada ya wanamuziki
wenzake Kikumbi Mwanza
Mpango na Juma Kakere kuingiza vipande vipya vya
mashairi katika wimbo wa
Jumbe 'Siri ya Nini' ambavyo vilimsisimua na
kujikuta akilia kwa furaha.
"Kiki na Kakere wameniliza kwakweli
sikutegemea kama wangeweza kunishtua
kwa kiasi hiki kwa namna walivyoingiza hisia
mpya kwenye wimbo huu na
kuifanya Remix kunoga,nimelia kwa furaha
kwakweli".
Alisema, walikuwa wakiufanyia mazoezi wimbo huo
bila kupangilia kama
wangeongeza kitu chochote lakini kwa namna
kombinesheni ya watatu hao
ilivyonoga atalazimika kuingia nao studio
kuurekodi upya.
Mastaa hao dansi wako kambini wakijifua
kujiandaa na mpambano dhidi ya
bendi ya Msondo Ngoma utakaofanyika Sept.2 mwaka
huu katika Ukumbi wa
Travertine Magomeni jijini Dar es Salaam.


Post a Comment