SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MCHAKA MCHAKA VPL KUENDELEA WIKIENDI HII
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita. Kwa muj...
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.
Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na  mechi moja.
Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Wakati tukimuombea njaa ndala sisi tujipange kumfumua a Lyon jumapili

    ReplyDelete
  2. Mchezo mgumu sana hasa yanga anapotutangulia kucheza, kila la kheri wekundu wa Msimbazi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yah ni kweli maana yanga lazima wafanye fitna,kikubwa kujipanga kikubwa tu

      Delete

 
Top