Mjumbe wa kamati ya utendaji Salum Mkemi amesema Klabu ya Yanga imesikitishwa sana na kitendo cha Bodi ya ligi kuipa Simba pointi tatu kufuatia rufaa waliyomkatia beki wa timu ya Kagera suger Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Mkemi alisema Yanga haina tena imani na watendaji wote wa Bodi ya ligi kwakitendo walichofanya kushindwa kuwa na kumbu kumbu mpaka kuanza kutafuta ushahidi kwa waamuzi.
"Viongozi wote wa bodi ya ligi wanatakiwa wajiuzulu kwasababu wametia aibu kwenye soka letu, hatuwezi kwenda Mahakamani kwasababu tunajua sheria za FIFA zinakataza kesi za mpira kupelekwa mahakama za kiraia lakini kama atatokea mwanachama akasema anaenda Mahakamani ni maamuzi yake binafsi,"alisema Mkemi.
Wakati huo huo Mkemi ameitaka kamati ya hadhi sheria na haki za wachezaji itolee ufafanuzi kesi ya Mchezaji Venance Ludovick wa African Lyon ambaye amesimamishwa kucheza kutokana na matatizo ya usajili na timu yake ya zamani Mbao FC.
"Sisi tulipeleka malalamiko yetu juu ya Mchezaji Ludovick kesi yetu ikapelekwa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji lakini mpaka leo hakuna maamuzi yaliyo amuliwa mchezaji huyo amesimamishwa kuendelea kucheza ligi, tunataka walitolee ufafanuzi haraka,"alisema Mkemi.
Jana kamati ya masaa 72 iliipa Simba pointi tatu na magoli matatu baada ya kubaini Kagera ilimchezesha mchezaji hiyo akiwa na kadi tatu za njano.
Wameze ndimu ,Simba mbele kwa mbele
ReplyDelete