Nyasi za uwanja wa Etihad kuanzia saa moja na nusu usiku wa leo zitakuwa katika wakati mgumu pale wenyeji Man City watakapowakarikibisha majogoo wa jiji la Liverpool, katika mchezo mkali wa ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama EPL.
Timu zote zitaingia uwanjani kwa lengo moja la kupata ushindi ili kuendelea kujikita katika nafasi ya kubaki ndani ya top four huku zikiendelea kuifukuzia Chelsea iliyozidi kupaa kileleni, kufuatia ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Stoke jana.
Record ya Liverpool dhidi ya timu zilizo kwenye top six inatisha kwani imefanikiwa kukusanya points 19 katika michezo 9 na huku record yake dhidi ya Manchester City ikiwa ya kuvutia zaidi kwani katika michezo iliyopita, Liverpool imeshinda mechi 5 na Man City wameshinda mechi 1 tu. Hii inafanya pambano hili kuwa gumu kwani Man City ambayo imetoka kuondoshwa kwenye michuano ya Uefa na Monaco itahitaji kupata ushindi ili kuiacha Liverpool ambayo wamepishana kwa pointi moja na nafasi moja. Timu Man City ina pointi 56 katika nafasi ya 3 huku Liverpool akiwa na pointi 55 katika nafasi ya 4.
Makocha wote wawili Pep Guardiola na Jurgen Klop waliongea na media kuelekea mechi hii na haya ndio maoni yao.
Guardiola: Itakuwa ni mechi ngumu lakini lazima turudishe imani na kujiamini tena baada ya kutolewa kwenye michuano ya Uefa, hatutabadili staili yetu ya kushambulia lakini itatulazimu tujilinde vizuri pia, ni mechi ngumu kwetu na tukicheza kama tulivyocheza dakika 45 za kwanza dhidi ya Monaco tutakuwa katika hali mbaya sana.
Klop: Sidhani kama sisi ndio tunapewa nafasi kubwa ya kushinda pamoja na kuwa tuna rekodi nzuri katika mechi kama hizi. Ni ngumu sana kucheza na timu anayofundisha Pep, tutalazimika kujilinda kwa tahadhari huku tukishambulia kwa nafasi.
Majeruhi.
City wataendelea kuwakosa Ilkay Gundogan na Gabriel Jesus wakati nahodha Vincent Company anaweza kurudi uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.
Kwa upande wa Liverpool wao wataendelea kuwakosa captain wao Jordan Henderson na Daniel Sturidge, wakati Dejan Lovren na Roberto Firminho wakitarajia kurejea dimbani.
Mechi zingine Leo ni
Middlesbrough vs Man United
Southampton vs Tottenham Hotspurs
SUPER SUNDAY : MAN CITY vs LIVERPOOL
Title: SUPER SUNDAY : MAN CITY vs LIVERPOOL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nyasi za uwanja wa Etihad kuanzia saa moja na nusu usiku wa leo zitakuwa katika wakati mgumu pale wenyeji Man City watakapowakarikibisha m...


Post a Comment