Kikosi cha nyota 21 wa timu ya Taifa ya Tanzania ya
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kimeondoka jana
alfajiri Septemba 5, 2016 kwa kwenda jijini Victoria, kwenye Kisiwa cha Mahe
nchini Shelisheli kwa ajili ya kupiga kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya
Congo-Brazzaville utakaofanyika Septemba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Serengeti Boys itacheza na Congo-Brazzaville katika
mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam kuwania nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali
za vijana zitafanyika mwakani nchini Madagascar.
Itakumbukwa kwamba Benchi la ufundi lilimshauri Rais wa
TFF, Jamal Malinzi kwamba kambi hiyo ipigwe Shelisheli. Hii ni mara ya pili kwa
Malinzi kutimiza ahadi yake kwa wachezaji hao. Kwa mara ya kwanza aliahidi
kuwapa kambi ya nje kama wangewatoa Shelisheli.
Timu kweli ilikwenda Madagascar kabla ya kuivaa Afrika
Kusini ‘Amajimbos’ na kuitoa na kwa sasa inakwenda Shelisheli kujipanga kwa
ajili ya kuitoa Congo-Brazzaville katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza
Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.
Post a Comment