SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: ALIECHEZESHA SIMBA NA YANGA KUCHEZESHA MCHEZO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA WANAWAKE CAIRO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mwamuzi wa kike wa Kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha ...
Mwamuzi wa kike wa Kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake  wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q 17) mwishoni mwa mwezi huu.

Jonesia Rukyaa atakua mwamuzi wa akiba katika mchezo huo kati ya Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa jijini Cairo wikiendi ya tarehe 25,26,27 Machi, 2016.

Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakua ni Carolyne Wanjala (Kenya), akisaidiwa na Carolyne Kiles (Kenya), Mary Njoroge (Kenya), huku kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Leah Annette Dabanga kutoka nchi ya Afrika ya Kati.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top