Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) inatarajiwa kuwasili leo alhamis saa
nne usiku kwenye uwanja wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege
binafsi tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania siku ya jumamosi uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Nigeria (NFF), kupitia kwa Toyin Ibitoye
msafara huo unatarajiwa kuwa na wachezaji 23 pamoja na viongozi wa benchi la
ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Sunday Oliseh pamoja na viongozi wengine
waandamizi wa shirikisho hilo.
Nigeria inatarajiwa kufanya mazoezi siku ya ijumaa saa 10 jioni katika
uwanja wa Taifa, ikiwa ni mazoezi mepesi ya kuelekea kwenye mchezo huo.
NIGERIA KUWASILI LEO TAYARI KUIVAA STARS
Title: NIGERIA KUWASILI LEO TAYARI KUIVAA STARS
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) inatarajiwa kuwasili leo alhamis saa nne usiku kwenye uwanja wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kw...


Post a Comment