Kalaghe Secondary School Kalaghe Secondary School Author
Title: MZEE YUSSUF ASEMA BUNGE HALITAMZUIA KUITUMIKIA JAHAZI
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Mfalme wa taarab hapa nchini, Mzee Yussuf amethibitisha kwamba ni kweli atawania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao lakini akatoa angalizo kuw...
Mfalme wa taarab hapa nchini, Mzee Yussuf amethibitisha kwamba ni kweli atawania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao lakini akatoa angalizo kuwa hiyo haimaanishi kuwa anaacha muziki. Akiongea katika onyesho la bendi yake ya Jahazi Modern Taarab Jumapili iliyopita katika ukumbi wa Travertine, 

Mzee alisema atachukua fomu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na iwapo kitampitisha basi atagombe ubunge katika jimbo Fuoni huko visiwani. “Nikiwa mheshimiwa bado nitaonekana kwenye maonyesho ya Jahazi, japo si sana, sidhani kama kuna kanuni itakayonikataza kuendelea na kazi yangu ya muziki,” alisema Mzee Yussuf.


 “Nitakuwa nakosekana wakati tu wa kwenda mjengoni au wasaa wa kwenda kuwatumia wapiga kura wangu lakini siku zingine tutakuwa pamoja. “Ila kama mnataka niendelee kutumbuiza kila siku, basi niombeeni dua nikose ubunge,” alisema Mzee na kusababisha mashabiki wengi kuangua kicheko. 

Msanii huyo ambaye majuzi alichukua tuzo tatu za Kilimanjaro Tanzania Music Awards, alibainisha kuwa siku zote ndoto zake zimekuwa ni kuwatumikia Watanzania katika kujikwamua kimaisha na hivyo anaamini ubunge ni njia nzuri ya kutekeleza azma yake.

 “Nikiwa mheshimiwa bado nitaonekana kwenye maonyesho ya Jahazi, japo si sana, sidhani kama kuna kanuni itakayonikataza kuendelea na kazi yangu ya muziki,” alisema Mzee Yussuf

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top