Kalaghe Secondary School Kalaghe Secondary School Author
Title: CHAN 2015: NOOIJ AONGEZA WACHEZAJI WATANO WA KUIPA NGUVU STARS
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
  Kocha mkuu wa timu ya Taifa Mart Nooij ameongeza wachezaji watano kwenye kikosi cha Stars kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi hi...
Kikosi cha Taifa Stars
Kocha mkuu wa timu ya Taifa Mart Nooij ameongeza wachezaji watano kwenye kikosi cha Stars kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi hicho ili kuziba pengo lililoachwa na wachezaji wa kimataifa ambao kutokana na kanuni hawaruhusiwi kucheza mashindano ya mataifa ya Afrika yanayoshirikisha wachezaji wa vilabu vya ndani maarufu kama CHAN.
Stars imewasili leo visiwani Zanzibar tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ kuwania kufuzu kwa mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani michuano itakayopigwa mwaka 2016 nchini Rwanda. Msafara wa Stars unajumuisha wachezaji 22 na benchi la ufundi lenye watu saba.
Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi cha Stars ni pamoja na Atupele Green, Rashid Mandawa, Hassan Dilunga, Hassan Isihaka pamoja na mchezaji chipukizi Kelvin Friday. Kocha anaamini kujumuishwa kwa wachezaji hao kutaongeza chachu ya ushindi kwenye mchezo huo ambao pia ni mtihani kwake kuhakikisha anaibuka na ushindi.
Afisa habari na mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznia (TFF) Baraka Kiuguto amesema, timu imewasili salama Zanzibar na leo usiku imefanya mazoezi kwenye uwanja wa Amaan kujindaa na mchezo wa Jumamosi thidi ya The Cranes.
“Timu imeshawasili Zanzibar tangu majira ya saa 5:00 asubuhi na imefikia katika hoteli ya Nungwi Inn na usiku wa leo imefanya mazoezi kwenye uwanja wa Amaan kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa siku ya Jumamosi dhidi ya Uganda  ‘The Cranes’ mchezo utakaochezwa majira ya saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki”, amesema Kizuguto.
“Mwalimu ameongeza wachezaji wengine watano, kama unavyojua tulivyoenda Misri tulikuwa na wachezaji wa kimataifa zaidi ya wanne ambao hawawezi kucheza CHAN akiwemo Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto, kwahiyo ilibidi mwalimu aongeze wachezaji wengine ili kutengeneza kikosi imara. Wachezaji walioongezwa ni Atupele Green, Rashid Mandawa, Hassan Dilunga, Hassan Isihak pamoja na mchezaji chipukizi Kelvin Friday”, Kizuguto aliwataja .
“Hao wachezaji watano walioongezwa wanajumuika na wachezaji wengine waliokuwepo kule Ethiopia na Misri, kwahiyo wanatengeneza kikosi cha wachezaji 22 watakao kuwepo kwa ajili ya mchezo wa keshokutwa”, ameeleza.
“Mwalimu amesema, kikubwa ni ushindi na anatambua kuwa watanzania wanahitaji ushindi na amesema watafnya vzuri”, ameongeza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top