Kamati inakutana kwa ajili ya kumalizia shauri la upangaji wa matokeo Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) kundi C inayozihusisha timu za Geita Gold, JKT Kanembwa, JKT Oljoro na Polisi Tabora.
Viongozi watakaohojiwa na Kamati ya Nidhamu ni, Yusuf Kitumbo (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora), Fateh Remtullah (Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabaora), viongozi wa benchi la ufundi Polisi Tabora, Mrisho Selemani, Boniface Komba, Bernard Rabiamu.
Kamati pia itawahoji Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita, Salum Kurunge na mwenyekiti wa Klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita.
Hii kamati iache danadana, inasemekana ushahidi wote uko wazi hadi audio za maelekezo zipo sijui kwanini wanapata kigugumizi
ReplyDelete