Mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid, Filipe Luis amesema euro milioni 100 za kumuuza nyota wao Antoine Griezmann itakuwa ni pesa ndogo kulinganisha na uwezo wake.
Griezmann amehusishwa kutimkia Barcelona mwishini mwa msimu ingawa mabingwa hao wa La Liga wamewakasirisha Atletico kwa njia wanazotumia kumshawishi nyota huyo.
Raia huyo wa Ufaransa ana kipengele kinachoruhusu kuondoka klabuni hapo kwa euro milioni 100 huku mkataba wake ukimalizika mwaka 2022.
"Griezmann kwa euro millioni 100 ni pesa kidogo kulinganisha na uwezo wake huo ndio ukweli, nadhani kama ataondoka itakuwa baada ya fainali ya Europa.
"Kila mtu anahitaji kushinda mchezo huu wa fainali vitu vingine vitafuata baadae," alisema Filipe Luis.
Griezmann 27, amefunga mabao 27 katika michuano yote msimu huu ambapo ndani ya miaka minne mfululizo amefunga zaidi ya mabao 25.
FILIPE LUIS ASEMA EURO MILIONI 100 KWA GRIEZMANN NI KIDUCHU
Title: FILIPE LUIS ASEMA EURO MILIONI 100 KWA GRIEZMANN NI KIDUCHU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid, Filipe Luis amesema euro milioni 100 za kumuuza nyota wao Antoine Griezmann itakuwa ni pesa ndogo ku...


Post a Comment