Katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Aprili 17 nchini Ethiopia Yanga itahitaji sare au ushindi wowote ili kufuzu hatua hiyo.
Kiungo Raphael Daud aliifungia Yanga bao la mapema sekunde ya 30 kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Hajji Mwinyi.
Dicha walicheza kwa umakini mkubwa wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza ambayo hayakuwa na madhara kwa Yanga.
![]() |
Ibrahim Ajib akiwatoka wachezaji wa Wolaita Dicha |
Emmanuel Martin aliifungia Yanga bao la pili kwa kichwa dakika ya 54 baada ya kumalizia krosi ya Mwinyi upande wa kushoto.
Mlinzi Andrew Vincent 'Dante' alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 70 baada ya kupata maumivu ya mguu.
Yanga iliwatoa Dante, Thaban Kamusoko na Raphael nafasi zao zikachukuliwa na Nadir Haroub, Pato Ngonyani na Juma Mahadhi wakati Dicha ilimpumzisha Temesgen Duba na kumuingiza Ayob Alemayenu.
Post a Comment