SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MTOGO WA DICHA AAHIDI KWENDA KUIMALIZIA YANGA ETHIOPIA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliji Arafat Djako wa Wolaita Dicha amesema bado wana nafasi ya kuitupa nje Yanga katika mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho ...
Mshambuliji Arafat Djako wa Wolaita Dicha amesema bado wana nafasi ya kuitupa nje Yanga katika mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho la Afrika utakaopigwa nchini Ethiopia.

Dicha itahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili kutinga hatua ya makundi baada ya jana kulala mabao 2-0 mbele ya Yanga.

Djako raia wa Togo ameiambia SDF Sports kuwa wana uwezo wa kugeuza matokeo katika mchezo wa marudiano nyumbani kwao Aprili 17.

"Tumekubali kufungwa lakini nasi tunaweza kuwafunga Yanga nyumbani, bado tuna nafasi ya kuvuka hatua ya makundi," alisema Djako.

Dicha imefika hatua hiyo baada ya kuzitoa timu za Zimamoto ya Zanzibar hatua ya awali na Zamelek ya Misri hatua ya kwanza ya kombe ya michuano hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top