Azam yenye pointi 45 ingeshinda ingefikisha alama 48 na kuishusha Yanga ambapo ingeizidi alama mbili na kudiwa moja na vinara Simba.
Azam wameingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa kwenye michuano ya FA na Mtibwa Sugar mwisho wa mwezi uliopita.
Katika mchezo wa leo Azam ilitengeneza nafasi kadhaa huku mshambuliji Shaban Idd akipoteza ya wazi kipindi cha kwanza.
Wenyeji City walitengeneza mashambulizi kupitia upande wa kushoto lakini hawakufanikiwa kupata bao.
City imeendelea kubaki nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 26.
Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa leo
Stand United 3-1 Njombe Mji
Ruvu Shooting 0-0 Tanzania Prisons
Ndanda FC 1-1 Kagera Sugar
Post a Comment