SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: AISEE! MOURINHO AFUNGWI MARA MARA MBILI, CITY YALALA ETIHAD
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha Jose Mourinho amekataa kufungwa mara mbili baada ya kuiwezesha Manchester United kiubuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Manchester...
Kocha Jose Mourinho amekataa kufungwa mara mbili baada ya kuiwezesha Manchester United kiubuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa ligi uliofanyika uwanja wa Etihad.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza United ilipoteza kwa mabao 2-1 katika mtanange uliofanyika uwanja wa Old Trafford.

City ilicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata mabao mawili ya haraka dakika ya 25 na 30 yaliyofungwa na Vincent Kompany na Illkay Gundogan.

United ilienda mapumziko ikiwa haijapiga shuti hata moja wakati City ikipiga mashuti saba.

Paul Pogba ambaye kipindi cha kwanza hakuwa kwenye kiwango bora aliisawazisha mabao yote mawili dakika za 51 na 53.

Mlinzi Chris Smalling aliifungia United bao la ushindi dakika ya 69 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa Alexis Sanchez.

Endapo City ingepata ushindi kwenye mchezo huo ingetawazwa mabingwa wapya wa EPL msimu wa 2017/18.

United imefikisha pointi 71 na kuendelea kujikita nafasi ya pili ya kwenye msimamo wakiwa na nyuma kwa alama 13.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top