Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney ameamua kustaafu katika soka la kimataifa baada ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachomenyana katika mechi za kufuzu kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Everton aliombwa na meneja wa timu ya soka ya Uingereza kushiriki katika mechi dhidi ya Malta na Slovakia.
''Kila mara nilipochaguliwa ilikuwa fahari kubwa kwangu lakini naamini imefikia muda wa kujiondoa'' , alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amefunga mabao 53 katika mechi 119 za kimataifa.



Post a Comment